Sisi ni kundi la wanasheria na mashirika ya kisheria katika Kijiji cha Vancouver ambao tumeunganika pamoja na kutoa msaada wetu kwa Waislamu au wale wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu katika Jimbo la B.C ambao wamekuwa chini ya ubaguzi na mashambulizi. Tunataka wale ambao wamepata mateso kutoka aina hizi mbalimbali za ubaguzi kwa sababu ya imani yao na/au asili yao tunawajulisha kwamba kuna wanasheria katika Jimbo la B.C ambao wanania ya kuwasaidia, wanasheria hao wana majukumu makubwa ya kukabiliana na wahalifu hao kupitia taasisi za kisheria
Access Pro Bono imeanzisha simu maalumu ambapo watu wanaweza kuwapigia kwa misingi ya siri, ukazungumza na wakili ukatowa malalamiko kuhusu ubaguzi au uhalifu wa chuki bila malipo. Sisi pia tutaufatilia na kuweka kumbukumbu, bila kumfichuwa alieleta habari ya aina ya malalamiko ambayo yalitotolewa kupitia simu hii maluum.
Ushauri wa kisheria utakua wa siri na wa bure kama wewe kujisikia kwamba umekuwa umebaguliwa, umenyanyaswa, au umekabiliwa na vurugu kwa sababu wewe ni Muislamu au walikuwa wanajua kama wewe ni Muislamu.
Supporting Organizations








